Simba Yaomba Kukabidhiwa Kombe May 23


SIMBA inafahamu kuwa Sevilla ni klabu kubwa duniani na itacheza nayo Mei 23, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar hivyo uongozi wao umeomba siku hiyo ukabidhiwe kombe la Ligi Kuu Bara.



Mechi hiyo ya kirafi ki imeandaliwa na Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya SportPesa ambao ni wadhamini wakuu wa Simba, na hii itakuwa mara ya kwanza Sevilla inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’ kutua Tanzania na kucheza mechi kwenye Uwanja wa Taifa.



Kwa sasa Simba ipo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bongo ikiwa na pointi 81 baada ya kucheza mechi 31 huku
ikifuatiwa na Yanga yenye 80 ikiwa imecheza michezo 34, timu hizi zote jana zilitarajiwa kucheza mechi za muendelezo wa ligi kuu.



Kutokana na viporo ilivyonavyo, Simba inatakiwa kushinda mechi zake tano zilizobaki ili iweze kutetea ubingwa wake na kabla ya kukutana na Sevilla itakuwa imeshacheza na kama watashinda zote basi watakuwa na pointi ambazo hazitaweza kufi kiwa na timu yoyote.


Akizungumza na Championi Jumamosi, jana Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Simba, Haji Manara alisema kuwa, kwa upande wao wamejipanga vizuri kuelekea katika mchezo huo huku ombi lao kwa Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ ni kuweza kuwapa kombe siku ya mechi yao na Sevilla.

“Kwanza niwashukuru SportPesa kwa nafasi hii waliyotupa kwa sababu kigezo walichotumia ni kufanya vizuri katika michuano SportPesa Super Cup na sisi tulifanya vizuri na hata ikitokea tena SportPesa Super Cup itabidi tufanye vizuri zaidi ili nafasi kama hizi zikitokea basi tupewe.
“Nilikua naangalia katika takwimu zangu kwamba tangu nizaliwe haijawahi kutokea kwa timu inashiriki La Liga kuja kucheza nchini, SportPesa wanatuandikia historia hivyo mashabiki wetu waje kwa wingi na tunawaomba wenzetu wa shirikisho maana kanuni haziwabani kama hawatajali watupe kombe letu mbele ya Sevilla kwa sababu kabla ya mechi hiyo tutakuwa tumeshatwaa ubingwa.

“Unajua itapendeza kwa sababu mchezo huo utakuwa unaangaliwa na dunia nzima, (TFF) tukabidhini kombe kwenye mechi hiyo kama ikiwapendeza na wakiona inafaa maana ni heshima na Wazungu wanapenda vitu kama hivyo,” alisema Manara.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad