Spika Ndugai aeleza sababu kuu ya kumwita Stephen Masele nyumbani
0
May 18, 2019
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kuwa Stephen Masele hajaitwa sababu ya migogoro inayoendelea Bunge la Afrika bali ameitwa sababu ya utovu wa nidhamu maana matendo yake anayofanya yanaliabisha Taifa
Spika Job Ndugai akihojiwa na BBC amesema hadi jana Masele hakuwa ameitikia wito wake, huku akieleza kuwa suala la kuitwa Kamati ya maadili ni haki yake ya kusikilizwa maana hatua za kinidhamu zinaweza kuchukuliwa bila kuitwa.
Ameendelea kusema kuwa akishafika Bungeni ndio Watanzania watajua kosa lake ni nini. "Lazima afike Bungeni mbele ya kamati ya maadili ili kujibu tuhuma zinazomkabili," amesema.
Utakumbuka hapo juzi Spika Job Ndugai alisema kuwa amemuandikia barua Rais wa PAP ya kusitisha uwakilishi wa Stehen Masele hadi Kamati ya Maadili itakapokamilisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.
Tags