Spika Ndugai aibana serikali kuhusu ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo

Spika wa Bunge Job Ndugai amesema ujenzi wa bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani ukikamilika utakuwa na tija kubwa kwa nchi kuliko ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) unaojengwa.

Akizungumza leo Bungeni  ameitaka Serikali kueleza kwa nini ujenzi wa mradi wa Bandari ya Bagamoyo haujengwi licha ya mzabuni kupatikana kutoka nchini China

Amemtaka Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe pindi atakapokuwa akihitimisha mjadala wa bajeti yake leo Jioni kutoa ufafanuzi wa suala hilo.

Spika Ndugai amesema hayo leo bungeni ambapo ameeleza kuwa kukamilika kwa reli ya SGR bila kuwa na bandari ya kisasa kama hiyo ambayo ilikuwa ijengwe Bagamoyo ni kazi bure kwani mpaka sasa nchini hakuna bandari nzuri hivyo Serikali inapaswa kuliona hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad