Sudan: Jeshi linataka sheria ya Kiislam iwe muongozo wa sheria nchini

Baraza la jeshi linaloongoza nchini Sudan linasisitiza kuwa Sheria ya dini ya Kiislam itasalia kuwa muongozo wa sheria mpya za nchi hiyo.

Viongozi wa waandamanaji wamewasilisha orodha ya mapendekezo wanayotaka yazingatiwe na serikali ya mpito baada ya rais Omar al-Bashir kuondolewa madarakani mwezi Aprili.

Lakini baraza hilo lenye wanachama 10 limesema kuwa "lina mashaka" na mapendekezo hayo- linadai waandamanaji wamekuwa ''kimya kuhusu sheria ya Kiislam''.

Mambo 3 muhimu unayohitaji kuyafahamu katika uchaguzi mkuu Afrika Kusini
Iran yajiondoa kwenye mkataba wa nyuklia
Uzito wa kupindukia waleta hofu Tanzania
Mazungumzo kati ya jeshi na upinzani yamekwama.

Luteni-Jenerali Shamseddine Kabbashi, ambaye ni msemaji wa baraza la mpito la jeshi lililochukua uongozi baada ya Bw. Bashir kutimuliwa uongozini, amaewaambia wanahabari kuwa wamekubaliana na mapendekezo yote yaliyotolewa na waandamanaji.

Hata hivyo ameongeza kuwa mapendekezo hayo, "hayakugusia chanzo cha sheria, na kwamba sheria ya dini ya Kiislam itasalia kuwa muongozo wa kutunga sheria mpya".


Waandamanaji wa Sudan wakifungua mfungo wao nje ya makao makuu ya jeshi mjini Khartoum siku ya pili ya Ramadan
Katiba ya sasa ya Sudan inasema kuwa sheria ya kiislam ndio muongozo wa maadili ya taifa.

Hata hivyo chini ya utawala wa Bw. Bashir sheria hiyo ilitumika kibaguzi na wanaharakati walikuwa wakisema inawalenga wanawake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad