Sudan yameahirishwa kwa mara nyingine huku pande zinazozungumza zikishindwa kupata muafaka kuhusu muundo wa baraza hilo la mpito kabla ya uchaguzi.
Baraza la mpito la kijeshi na wawakilishi wa makundi ya upinzani nchini Sudan wameshindwa tena kuafikiana kuhusu kuundwa kwa chombo kipya kitakachotawala taifa hilo, wakati mazungumzo baina yao yakikabiliwa na mkwamo kuhusu watawala wa chombo hicho, kati ya wanajeshi ama raia.
Baraza hilo le kijeshi na wawakilishi hao wa makundi ya upinzani walikutana tena kwenye kasri la rais kuanzia Jumatatu jioni kuhitimisha mapendekezo ya muundo wa chombo hicho, lakini hawakufanikiwa kufikia makubaliano.
Hakuna upande uliozungumzia kuhusu kurejea kwa mazungumzo hayo, lakini mmoja wa viongozi wa waandamanaji Siddiq Yousef aliwaambia waandishi wa habari kwamba mazungumzo yalisitishwa tena hadi kutakapopatikana suluhu kati yao na baraza na kijeshi.
Afrika | Protests im Sudan (picture-alliance/dpa/AA/M. Hjaj)Waandamanaji nchini Suda wanataka serikali ya mpito ya kiraia.
Hata hivyo baraza hilo halitoa tamko lolote kuhusu kuahirishwa kwa mazungumzo hayo. Lakini kulingana na taarifa ya pamoja iliyotolewa na wawakilishi wa jeshi na makundi hayo usiku wa jana baada ya majadiliano hayo kusitishwa ilisema suala moja kubwa ambalo bado linazozaniwa linahusiana na mgawanyo wa wawakilishi wa kijeshi na raia kwenye baraza hilo, na nani atakuwa kiongozi wa baraza hilo jipya.
Kiongozi maarufu wa Muungano wa Freedom and Change Satea al-Haj amesema baraza la kijeshi linasisitiza kwamba rais wa baraza hilo huru anatakiwa kutoka jeshini, na kukataa kiongozi wa kiraia. Awali al-Haj alisema, wanahalalisha hilo kwa kudai kwamba taifa hilo linakabiliwa na vitisho vya kiusalama. Kulingana na al-Haj, jumuiya ya kimataifa haitakuwa tayari kushirikiana na serikali ya kijeshi.
Pande hizo mbili zilianzisha raundi ya pili ya mazungumzo Jumapili jioni kuhusu baraza litakalotawala Sudan katika miaka mitatu ya mpito, kufuatia kuondolewa kwa aliyekuwa rais Omar al-Bashir.
Sudan Mambo Bado Magumu Pande Mbili Zashindwa Kuafikiana
0
May 21, 2019
Tags