Thabit madai.
Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) imeangamiza jumla ya Tani 183 za bidhaa mbalimbali za chakula na dawa kutokana na kuisha muda wake na kukosa ubora kwa matumizi ya Binadamu.
Bidhaa zilizoteketezwa ni mchele tani 163 uliofeli vipimo vya maabara na uliongizwa nchini na Kampuni ya Zenj General Marchandize Ltd na unga wa ngano tani sita ulioharibika baada ya kuingia maji ya mvua.
Bidhaa nyengine ni tende tani tano, vipodozi tani moja, juice na bidhaa mchanganyiko vyote vikiwa vimemaliza muda wa matumizi ya binadamu.