Ikiwa leo ni siku ya Uhuru wa Habari duniani, Tanzania imeporomoka kwa nafasi 25 katika viwango vya Uhuru wa Habari Duniani hadi nafasi ya 118 kwa mwaka 2019 kutoka nafasi ya 93 mwaka 2018 kati ya nchi 180
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka (Reportes Without Borders), sekta ya habari nchini Tanzania imekumbana na changamoto mbalimbali kufuatia kupitishwa kwa sheria inayoonekana kuwa kandamizi, kufungwa kwa vyombo vya habari, na kufukuzwa kwa wanahabari nchini
Kwa mujibu wa ripoti hiyo mambo mengine yaliyochangia Tanzania kuporomoka kwa kiwango hicho ni tukio la kuvamiwa kwa Clouds Media Group mwaka 2017, kufungiwa kwa baadhi ya vyombo vya habari na waendeshaji wote wa tovuti na blogu za habari kutakiwa kujisajili na kulipa ada ili kuweza kutoa huduma hiyo
Matukio yaliyotikisa sekta ya habari ni kukamatwa watumishi wawili wa Tume ya Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ), Novemba 2018 ambao walikuja nchini kufahamu changamoto zinazowakumba waandishi wa habari
Aidha, tukio jingine ni kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa mwandishi wa kujitegemea, Azory Gwanda aliyekuwa akichunguza mauaji ya viongozi wa Serikali za mitaa mkoani Pwani - #regrann