Trump atangaza dharura kulinda mawasiliano ya nchi dhidi ya maadui

Rais Donald Trump ametangaza hali ya dharura kwa ajili ya kuilinda mifumo ya kompyuta dhidi ya '' wapinzani wa kigeni''

Rais huyo wa Marekani amesaini sheria ya utaratibu wa utendaji ambayo inazuwia mara moja makampuni ya Marekani kutumia mawasiliano ya kigeni yanayoaminiwa kuhatarisha usalama wa nchi hiyo.

Muasisi wa Huawei Ren Zhengfei aliwahi kusema kuwa Marekani haiwezi kumaliza biashara zake
Hata hivyo, wachambuzi wanasema uamuzi huo unailenga kampuni kubwa ya mawasiliano ya Kichina Huawei.

Nchi kadhaa- Marekani ikiwemo-zimekwisha elezea wasi wasi wake kwamba huduma za kampuni hiyo zinaweza kutumiwa na Uchina kwa upelelezi. Huawei imesema kuwa kazi yake haisababishi tisho lolote.

Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu ya White House, agizo la Bwana Trump linalenga "kuilinda Marekani dhidi ya wapinzani wake ambao wamekuwa wakionekana kubuni mbinu za kutumia taarifa na mifumo ya teknolojia ya mawasiliano pamoja na huduma zake ".

Sheria hiyo ya rais inampatia mamlaka waziri wa biashara nchini humo ya "kuzuwia shughuli zinazohatarisha hatari isiyokubalika kwa usalama wa taifa ", iliongeza taarifa.

Hatua hiyo iliafikiwa mara moja na mwenyekiti wa Tume ya kitaifa ya mawasiliano Ajit Pai, ambaye amesema katika taarifa yake kwamba ilikuwa ni "hatua muhimu kuelekea kuilinda mitandao ya Marekani ".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad