Trump Atangaza Ushuru Dhidi ya Mexico

Trump Atangaza Ushuru Dhidi ya Mexico
Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza ushuru wa asilimia tano kwa bidhaa zote zinazotoka nchini Mexico, ili kuishinikiza nchi hiyo kuzuia wahamiaji haramu kuingia Marekani.

Katika taarifa yake, Trump amesema ushirikiano wa Mexico usiokuwa na vitendo vya kuzuia mmiminiko wa wahamiaji haramu ni tishio kwa usalama wa kitaifa na uchumi wa Marekani.

Trump ameongeza kwamba ushuru huo utaanza kutozwa rasmi kuanzia Juni 10, na utaongezwa hadi asilimia 10 ifikapi Julai mosi iwapo mgogoro huo utaendelea kuwepo.

Tamko la Trump la kushangaza linakuja huku Marekani, Mexico na Canada wakijaribu kufikia makubaliano ya biashara huru. Haijulikani iwapo mkataba huo wa biashara utaathirika kutokana na hatua ya Trump.

 Thamani ya biashara kati ya Mexico na Marekani ilifika dola bilioni 671 mwaka jana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad