Mbunge wa Singida Mashariki kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amebainisha kuwa atarudi nchini, Septemba 7, 2019 ili aweze kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyia mwishoni mwa mwaka huu.
Lissu ambaye alishambuliwa kwa risasi Septemba 7, 2017 akiwa kwenye vikao vya Bunge jijini Dodoma amesema baada ya kukamilisha matibabu yake mwezi wa 6 mwaka huu atahakikisha anarudi nchini kwa ajili ya kuendelea na shghuli zake za kisiasa.
Lissu amesema kuwa, "narudi nyumbani siku ya Septemba 7 anniversary ya kushambuliwa kwangu."
April 18, 2019 Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki alisema kuwa, "May 14, 2019 nitapimwa urefu wa miguu ili nitengenezewe kiatu maalum kwa ajili ya mguu wa kulia, kwa sababu ya majeraha makubwa niliyopata, bila kiatu au soli maalum nitakuwa 'langara' sana na madaktari wamesema hiyo sio sawa sawa, pia nina tarehe ambayo madaktari wangu wamesema nitakuwa 'fiti' kurudi nyumbani."
"Msiniambie niseme kwa wakati huu nahitaji kushauriana na wadau kuhusu tarehe halisi na namna bora zaidi ya kurudi kwangu nyumbani, Kwa hiyo, wakati muafaka utakapofika, nitawaeleza tarehe kamili ya kurudi nyumbani na kwa mlioko Dar es salaam, mniandalie supu ya utumbo wa mbuzi." aliandika Lissu.