Mamlaka ya Afya nchini imepata hofu ya ongezeko la watu wenye uzito mkubwa.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto, Faustine Ndugulile amesema kuwa sasa ni zaidi ya asilimia kumi ya watanzania wanasumbuliwa na tatizo hilo la uzito wa kupindukia.
Waziri huyo ameainisha kuwa ongezeko la kuenea kwa magonjwa yasiyoambukiza imeleta changamoto na kutoa tahadhari kuwa idadi hiyo kubwa inaweza kusababisha madhara makubwa kwa wananchi.
Aidha ameainisha kuwa tatizo la uzito uliopindukia ni kubwa kwa wanaume na wanawake wa maeneo ya mjini kuliko Vijijini.
Huku changamoto ya vyakula vyenye virutubisho kuongeza kasi ya tatizo hilo kwa kiwango kubwa .
Naibu Waziri Ndugulile alieleza hayo wakati anajibu swali la nyongeza lililoulizwa bungeni na Zainabu Mwamwindi aliyeuliza kama kuna uhitaji wa kuwawezesha maafisa wa lishe kwa sababu ya ongezeko la utapia mlo.