VIDEO: Wanaume wanaopigwa na wake zao watakiwa kupeleka malalamiko ya Polisi


Wanaume wanaopigwa, kunyanyaswa kingono na wake zao na ukatili mwingine wametakiwa kuripoti matukio hayo katika madawati ya jinsia yaliyopo vituo vya Polisi nchini.

Wito huo umetolewa na bungeni leo  na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Iringa, Rita Kabati (CCM).

Katika swali lake  Kabati aliuliza: Kwakuwa vitendo vya wanaume kupigwa , kunyanyaswa na wake zao vimeongezeka ni lini serikali italeta sheria ili kuwalinda wanaume hao?

Katika majibu yake, Dk. Ndugulile amesema sheria ya ukatili wa kijinsia haibagui nani amefanyiwa ukatili huo kati ya wanaume na wanawake, hivyo wanaume wanaopigwa na kufanyiwa vitendo vyovyote vya ukatili waripoti madawati ya jinsia yaliyopo vituo vya polisi.

==>>Tazama hapo chini
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad