Vinginevyo Mtatuona Wabunge Wabaya - Nape Nnauye Afunguka

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM), amewataka wabunge kuweka mguu sawa kuibana Serikali ili iongeze Bajeti kwenye Maji huku akisema vinginevyo watawaona Wabunge wabaya. 


Ameyasema hayo bungeni leo Mei 2, wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Maji ambapo amesema ataunga mkono bajeti hiyo endapo serikali italeta mpango mpya wa kuongeza fedha kwenye bajeti ya wizara hiyo. 


“Huu mfuko wa maji jadilianeni mnavyoweza hadi tuone kuna ongezeko la fedha za kutosha ili wananchi wetu vijijini wapate maji, vinginevyo mtatuona wabunge wabaya,” amesema Nape.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad