Wabunge 7 wa Chadema Kuvuliwa Uongozi Arusha

Kamati ya utendaji ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya Kaskazini imependekeza kwa Kamati Kuu kuvuliwa nafasi za uongozi wa chama Wabunge saba na kuvuliwa uanachama Meya mmoja wa jiji kutokana na makosa ya kinidhamu


Kamati hiyo pia imemvua uanachama Diwani Viti Maalumu katika jimbo la Arumeru Mashariki, Digna Nassari kwa tuhuma ya makosa ya kinidhamu na usaliti

-

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa amesema wamechukua uamuzi huo ili kukisafisha chama kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani


Hata hivyo, Golugwa aliomba kutotaja majina ya wabunge wanaopendekezwa kuvuliwa nyadhifa zao  - #regrann  

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad