Wachezaji wa Simba Wakishangilia Ubingwa.. Utabiri wa Mchungaji Mashimo Washindwa

Tayari Simba SC wamenyakua Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/19 baada ya kuichapa Singida United mabao 2-0 kwenye uwanja wa Namfua Singida. 


Kwenye ushindi huo magoli ya Simba yamefungwa na Meddie Kagere dakika ya 10, na John Bocco 60. Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 91 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwenye ligi msimu huu, ikiwa bado ina michezo miwili mkononi. 

Ikumbukwe Mchungaji maarufu mtandaoni anayejulikana kama Mchungaji Mashimo alitabiri kuwa Timu ya Simba kamwe haiwezi chukua Ubingwa mwaka huu lakini imekuwa kinyume chake








Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad