Wahadhiri Wa Kigeni Nchini Wapungua Kutoka 502 Na Kubakia 151 Pekee.
0
May 24, 2019
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Serikali imesema ,katika miaka 10 iliyopita kati ya Mwaka 2008/2009 hadi 2018/2019 vyuo vikuu 17 vya umma 8 na binafsi 9 viliajiri wanataaluma wa kigeni 502.
Hayo yamesemwa leo Mei 24,2019 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe.Mwita Waitara kwa niaba ya Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,wakati akijibu Swali la mbunge wa Nkenge Balozi Dkt.Diodorus Kamala aliyehoji ,Kumekuwepo na utaratibu wa kuajiri wahadhiri toka nje ya nchi kwa lengo la kukuza tafiti na taaluma katika vyuo hivyo je,katika miaka 10 iliyopita ,ni wahadhiri wangapi toka nje wameajiriwa katika vyuo vikuu Tanzania na ni mafanikio gani kitaaluma na kiutafiti yameletwa na wahadhiri hao toka nje ya nchi.
Katika Majibu yake,Mhe.Waitara amesema vyuo vikuu vimekuwa vikiajiri wanataaluma kutoka nje kwa malengo ya kuboresha hali ya Taaluma na kujiimarisha katika masuala ya kiutafiti katika Nyanja mbalimbali ambapo katika miaka 10 iliyopita kati ya mwaka 2008/2009 hadi 2018/2019 ,vyuo vikuu 17 [vya umma 8 na binafsi 9] viliajiri wanataaluma wa kigeni 502.
Aidha,Mhe.Waitara amesema kutokana na jitihada za serikali na vyuo vyenyewe kuendeleza wataalam wa ndani, wanataaluma wa kigeni wameendelea kupungua kutoka 502 na kubaki 151 tu hadi kufikia mwaka 2018/2019.
Hata hivyo,Naibu Waziri Waitara amesema mafanikio yaliyopatikana baada ya kuajiri wataalam wa kigeni ni pamoja na kupata wataalam wa fani ambazo nchi haijajitosheleza, kuanzishwa kwa Program mpya katika vyuo mbalimbali , kuongeza ushirikiano kati ya vyuo vya ndani na nje,na kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya kufundishia na kujifunzia ikiwa ni pamoja na vifaa vya maabara za utafiti.
Katika hatua nyingine Mbunge Kamala ameishauri Serikali kuona namna ya kubadilisha sheria ya kustaafu kwa wahadhiri wasiwe wanastaafu mpaka achoke mwenyewe ili kutatua upungufu wa Wasomi wahadhiri hapa nchini ambapo Naibu Waziri Waitara amesema maoni hayo Serikali imeyapokea na yatafanyiwa kazi.
Tags