Wahadhiri Wa Kigeni Nchini Wapungua Kutoka 502 Na Kubakia 151 Pekee.


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
 Serikali imesema ,katika miaka 10 iliyopita  kati ya Mwaka 2008/2009 hadi 2018/2019  vyuo vikuu   17 vya umma 8 na binafsi 9  viliajiri wanataaluma wa kigeni 502.

Hayo yamesemwa leo Mei 24,2019 bungeni jijini Dodoma na  Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe.Mwita Waitara  kwa niaba ya Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,wakati akijibu Swali la mbunge wa Nkenge  Balozi Dkt.Diodorus Kamala  aliyehoji ,Kumekuwepo na utaratibu wa kuajiri wahadhiri toka nje ya nchi  kwa lengo la kukuza tafiti  na taaluma katika vyuo hivyo  je,katika miaka 10 iliyopita ,ni wahadhiri wangapi toka nje   wameajiriwa  katika vyuo vikuu Tanzania   na ni mafanikio gani kitaaluma  na kiutafiti  yameletwa na wahadhiri hao toka nje ya nchi.

Katika Majibu yake,Mhe.Waitara amesema  vyuo vikuu vimekuwa vikiajiri wanataaluma  kutoka nje kwa malengo ya kuboresha hali ya Taaluma  na kujiimarisha  katika masuala ya kiutafiti  katika Nyanja mbalimbali  ambapo katika miaka 10 iliyopita  kati ya mwaka 2008/2009 hadi 2018/2019 ,vyuo vikuu 17 [vya umma 8 na binafsi 9] viliajiri wanataaluma wa kigeni 502.

Aidha,Mhe.Waitara amesema kutokana na jitihada za serikali na vyuo vyenyewe  kuendeleza wataalam wa ndani, wanataaluma wa kigeni  wameendelea kupungua  kutoka 502 na kubaki  151 tu  hadi kufikia mwaka 2018/2019.

Hata hivyo,Naibu Waziri Waitara amesema mafanikio yaliyopatikana baada ya kuajiri wataalam wa kigeni  ni pamoja na  kupata wataalam  wa fani ambazo nchi haijajitosheleza, kuanzishwa kwa Program mpya  katika vyuo mbalimbali , kuongeza ushirikiano kati ya vyuo vya ndani na nje,na kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kisasa  vya kufundishia na kujifunzia ikiwa ni pamoja na vifaa vya maabara za utafiti.

Katika hatua nyingine Mbunge Kamala ameishauri Serikali kuona namna ya kubadilisha sheria ya kustaafu kwa wahadhiri wasiwe wanastaafu mpaka achoke mwenyewe  ili kutatua upungufu wa Wasomi wahadhiri hapa nchini ambapo Naibu Waziri Waitara amesema maoni hayo Serikali imeyapokea  na yatafanyiwa kazi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad