Waingereza wanafanya mapenzi kwa kiwango kidogo tofauti na miaka ya nyuma

Siku za hivi karibuni imegundulika kuwa waingereza wanafanya mapenzi kwa kiwango kidogo tofaiti na miaka ya nyuma , kwa mujibu wa utafiti uliofanywa katika taifa hilo.

Utafiti huo umechapishwa katika jarida la 'British Medical' , a,mbapo umesema kuwa tatu ya nne ya wanawake na wanaume hawajafanya mapenzi mwezi uliopita.

Video za ngono zilivyokatisha maisha ya binti
Mitandao ya habari ya kijamii huwaathiri vijana
Idadi hiyo imeongezeka kwa takribani moja ya nne tangu mwaka 2001, kwa mujibu wa takwimu ya watu 34,000.

Zaidi ya nusu ya wanaume na wanawake wenye umri wa kati ya miaka 14 mpaka 44 wamefanya mapenzi wiki iliyopita, ripoti hiyo inaeleza.

Wapenzi wanaoishi pamoja au wanandoa , kiwango cha kufanya mapenzi kimeshuka zaidi.

Kupungua kwa ngono
Taarifa ambazo watafiti wameziangalia zimetoka kwa tafiti tatu zilizofanikiwa kufanywa na watafiti wa kitaifa wa nchini humo kuhusu tabia za watu na ushiriki wa ngono zilizofanywa mwaka 991, 2001, na 2012 .

Utafiti huo umetoa picha ya namna waingereza wanavyojihusisha na ngono.

Kwa mujibu wa tafiti za hivi karibuni:

Asilimia 41 ya watu wenye umri kati ya miaka 16 mpaka 44 huwa wanafanya mapenzi angalau mara moja kwa wiki mwezi uliopita
Uwiano wa ripoti wa watu kutoshiriki katika ngono katika mwezi uliopita imeongezeka kutoka asilimia 23 mpaka asilimia 29 miongoni mwa wanawake huku wanaume imeongezeka kutoka asilimia 26 mpaka 29.2 kati ya mwaka 2001 mpaka 2012
Idadi ya watu walioripotiwa kujihusisha na ngono mara kumi au zaidi imepungua mwezi uliopita kutoka asilimia 20.6 kufikia 13.2 kwa wanawake huku wanaume kiwango kikiwa kimeshuka kutoka asilimia 20.2 mpaka 14.4 kati ya mwaka 2001 na 2012

Wastani wa idadi ya watu wenye umri wa miaka 35 mpaka 44 kufanya mapenzi mwezi uliopita imepungua mwezi uliopita kutoka mara nne na kufikia mara mbili kwa wanawake na kwa wanaume imepungua kutoka mara nne mpaka mara tatu.
Kwa nini ngono imepungua?

Watafiti kutoka shule ya usafi na madawa ya kitropiki unasema kiwango cha ushiriki wa ngono wa mara kwa mara miongoni mwa watu ambao walikuwa wanafanya mapenzi kila wakati umepungua tofauti na idadi ya watu kuamua kuendelea kuhifadhi ubikira wao .


Ingawa watu wenye umri chini ya miaka 25 na wale ambao hawana wapenzi wanaonekana kuwa na unafuu katika kushiriki katika ngono, kiwango kimeshuka kwa wanandoa na watu wenye umri mkubwa au wapenzi wanaoishi pamoja kwa muda mrefu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad