Wanawake Wazidi Kuchanja Mbuga Kimaendeleo

Wanawake nchini, jana Jumatano katika kusherehekea siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) walidhihirishwa kuwa wako juu wakati wakitoa tuzo mbalimbali za wanawake wanaofanya vizuri katika fani mbalimbali ikiwemo mambo ya mazingira, afya, sheria, sayansi na teknolojia na mambo mengine.


Hayo yaridhihirika kwenye kongamano la thamani ya mwanamke na ajira binafsi lililoandaliwa na kampuni ya Purple Planet chini ya Mkurugenzi Hilda Kisoka na kufanyika Ukumbi wa King Solomoni uliopo Kinondoni, Namanga, Dar na kuhudhuriwa na mamia ya wanawake kutoka mikoa mbalimbali ya hapa nchini.


Mkurugenzi wa Taasisi ya HIDECA inayojihusisha na utunzaji wa mazingira ,Sara Pima (kushoto) akimkumbatia mshindi wa tuzo ya mazingira, Upendo Mmari.



Katika kongamano hilo mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Hanang mkoni Manyara Dk. Mary Nagu ambaye alishuhudia ugawaji wa tuzo mbalimbali kwa wanawake hao.



Miongoni mwa tuzo zilizotolewa kwenye kongamano hilo ni tuzo ya afya ambapo wanawake waliojitolea maisha yao kupigania afya za uzazi wa mpango, kupunguza maambukizi ya Ukimwi walitunukiwa tuzo.


Wanawake wengine walioibuka na tuzo hizo ni wanasheria waliowahi kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake wenzao na watu wengine wapotaka kupoteza haki zao kwa kukosa kipato.



Tuzo nyingine ilikuwa ni ya mazingira ambapo wanawake kadhaa waliofanikisha zoezi la utunzaji wa mazingira na kutoa elimu hiyo sehemu mbalimbali ikiwemo mashuleni sokoni na sehemu nyingine za mikusanyiko nao walitunukiwa tuzo.


Mkurugenzi wa Purple Planet, Hilda Kisoka akitoa shukrani zake kwa wote waliofanikisha kufanikiwa kwa kongamano hilo ambalo linafanyika kila mwaka.

Wakulima nao hawakuachwa kwani wanawake waliofanya vizuri kwenye sekta ya kilimo nao walitunukiwa tuzo.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na wanawake kutoka mikoa mbalimbali ya hapa nchini.

Kongamano hilo sambamba na kutawaliwa na shangwe na nderemo kwa waliokuwa wakipokea tuzo na wapambe wao.

Pamoja na shangwe hizo mwanamuziki mkongwe wa taarab, Patricia Hilary naye aliwanogesha wanawake hao kwa nyimbo zake zilizowahi kutamba kama ule wa Njiwa Peleka Salamu, Jamani Mapenzi Yananitatiza na Ni Mdodo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad