Baada ya Ligi Mbalimbali kumalizika kwa sasa mataifa mengi ya Afrika yanaelekeza nguvu katika fainali za mataifa ya Afrika AFCON 2019 zinazofanyika Misri, fainali hizo zimepangwa kuchezwa kuanzia June 21 zikiwa zinakutanisha jumla ya timu 24.
Timu ya taifa ya Senegal iliyopo Kundi C lenye timu za Tanzania, Algeria na Kenya tayari waziri wa michezo wa Senegal Matar Ba ametangaza kuwa Senegal wametengewa bajeti ya dola milioni 5.1 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 11.7.
Bajeti hiyo iliyotangazwa na waziri Matar Ba italenga katika kusaidia maandalizi ya timu hiyo inayotarajia kuweka kambi Hispania, Senegal inaonekana kutia nguvu zaidi kutokana na kutaka kutwaa taji lao la kwanza la AFCON katika historia yao.