Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi au Klynn
1
May 04, 2019
Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania.
Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000).
Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd .
Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi.
Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani.
Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike
Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu
Muziki
Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites.
Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu.
Mnamo mwaka 2004 alitoa kibao chake 'Nalia kwa Furaha'.
Mwaka 2007 alitoa albamu nyengine kwa jina 'Crazy over You' ambacho kilikuwa kibao cha kwanza cha albamu yake mpya.
Anasema kwamba umaarufu wake ulianza alipoanza kuimba.
Kulingana na mjasiriamli huyo muziki ndio uliokuwa ndoto yake kubwa akiwa mtoto .
Alitizama kanda za video za wanamuziki tajika kama vile Mariah Carey na Whitney Houston ili kujifunza kuimba
Malkia wa urembo
2000 Alichaguliwa malkia wa Urembo nchini Tanzania baada ya kushinda taji la malkia wa urembo la miss Ilala.
Alitumikia taji la miss Tanzania kwa mwaka mmoja akizishughulikia jamii mbalimbali
Katika kushiriki katika shindano hilo alishawishiwa na mmoja wa waandalizi wa shindano hilo kujaribu bahati yake.
Katika shindano la dunia lililofanyika nchini Uingereza , alikutana na watu tofauti waliokuwa na malengo tofauti ambapo anadai kujifunza mambo mengi tofauti
Tuzo alizoshinda
2007: Alishinda tuzo ya mwanamuziki bora wa kike pamoja Tanzania na kolabo bora kupitia wimbo wake Crazy over you
2007: Alishinda tuzo ya Mwanamuziki bora kutoka Pearl Music Award
2008: Alishinda tuzo nyengine ya mwanamuziki bora wa Tanzania
2008: Alipata tuzo ya Mwanamuziki bora wa kike Tanzania kutoka Pearl Music Awards
2013: Alishinda taji la mwanamke mwenye mitindo bora katika tuzo za fesheni za Swahili
2017: Alijishindia tuzo ya shaba ya kimatifa kwa jina, Sayari amp,
2017: Alijishindia tuzo nyengine ya shaba katika orodha ya samani kwa jina Ngorongoro settee,
Ndoa
Mwaka 2015 alifunga ndoa na Bilionea wa Tanzania Reginald Mengi, na wamejaliwa watoto wawili wavulana .
Marehemu mumewe ni mwenyekiti wa makampuni ya IPP nchini Tanzania
BBC
Tags
NI MWANAMKE MWENYE KULENGA MBELE, ANAJARIBU KUFUATA KILE ANCHOAMINI KUWA ANAWEZA NA ANAPENDA KUKIFANYA.
ReplyDelete