Watu 11 Wauawa Kwa Kupigwa Risasi Katika Shambulio Lililotokea Brazil

TAKRIBAN watu 11 wameuawa baada ya watu wenye silaha kuvamia baa moja na kuwashambulia kwa risasi watu waliokuwemo ndani ya baa hiyo iliyopo katika jimbo la Para kaskazini mwa Brazil.



Msemaji wa jimbo hilo, Natalia Mello, amesema washambuliaji hao waliokuja wakiwa kwenye magari na pikipiki waliwashambulia watu hao kabla ya kukimbia.


Mello amesema vifo hivyo vilihusisha wanawake sita na wanaume watano ambapo  polisi wamesema washambuliaji hao walikuwa saba, na mmoja alijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad