Takriban watu 17 wamefariki na wengine 44 wamelazwa katika hospotali mbili na wanaendelea kupokea matibabu baada ya kukunywa pombe bandia katika jimbo la Uttar Pradesh kaskazini mwa India.
Maafisa wa afya wameeleza kuwa baada ya kunywa pombe hiyo,wanakijiji walilalamika kutoona na kichefuchefu. Waziri wa idara ya Ushuru Jai Pratap Singh alisema kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale wanaopatikana na hatia ya kuuza pombe hiyo haramu.