Watu 80 Wamematwa Nigeria kwa Tuhuma za Kula Wakati wa Ramadhan

Polisi wa Sharia ya Kiislamu katika jimbo la kaskazini mwa Nigeria la The Islamic Sharia Kano wamewakamata kwa muda watu 80 walioshumiwa kwa kula hadharani, badala ya kufunga kuanzia alfajiri hadi jua linapotua kulingana na maagizo ya dini ya kiislamu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Polisi wa Sharia , wanaofahamika kama Hisbah, wanasema kuwa watu hao walikamatwa kwa nyakati tofauti katika maeneo mbali mbali ya mji wa Kano katika kipindi cha siku kadhaa.

Jimbo la Kano ni moja kati ya majimbo kadhaa ya kaskazini mwa Nigeria ambako Sharia ya kislamu ilianzishwa upya tangu mwaka 2000.

Sharia ya kiislamu inatekelezwa sambamba na sheria ya kawaidakwenye majimbo hayo.


Msemaji wa Hisbah katika jimbo la Kano, Adamu Yahaya, ameiambia BBC kuwa wote waliokamatwa walikuwa ni Waislamu na maafisa hawawalengi wasio Waislamu kwasababu hawafungwi na sheria ya kiislamu.

Amesema kuwa baadhi ya wale waliokamatwa waliiambia ofisi ya Sharia kuwa walikuwa wanakula kwasababu hawakuuona binafsi mwezi wa Ramadhani chuku wengine wakisema walikuwa ni wagonjwa, lakini maafisa walisema kuwa madai yao hayakuwa na msingi wowote.


Watu hao 80 walionywa na kuachiliwa huru kwasababu walikuwa wamefanya kosa hilo kwa ''mara ya kwanza'' alisema Bwana Yahaya.

Walionywa kuwa iwapo watakamatwa tena, watapelekwa mahakamani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad