Tangu kuzuka upya kwa ugonjwa huo mwezi Agosti mwaka jana, tayari umeshaingia kwenye kumbukumbu za dunia kwa kuwa ugonjwa wa pili kwa kuua zaidi duniani.
Vifo 994 vimeripotiwa lakini idadi hiyo iliongezeka hadi vifo1,000 baada ya wizara ya afya kuchapisha takwimu zake jana Ijumaa. Hadi sasa kuna taarifa rasmi 119 za kushambuliaa kwa vituo vya kupambana na Ebola pamoja na madaktari tangu mwezi Januari mwaka huu.
Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Michael Ryan amesema kutoaminiana na vurugu vimekuwa chanzo cha kukwama kwa jitihada za kuudhibiti ugonjwa huo unaosambaa kupitia upande wa mashariki wa nchi hiyo.