Rai hiyo imetolewa Mei 14,2019 jijini Dodoma na Naibu katibu mkuu Utumishi, Bw.Francis Michael katika ufunguzi wa mkutano Mkuu wa Mwaka wa Baraza la wafanyakazi wa ofisi ya Taifa ya Ukaguzi hesabu za Serikali C.A.G.
Bw.Michael amesema kuna baadhi ya watumishi wa Umma wamekuwa wakikiuka maadili ya kazi na taaluma zao na kujikita wakiwa watovu wa nidhamu na kujikita kwenye masuala ambayo yako kinyume na utaratibu wa kazi hivyo ni vyema kwa kila mfanyakazi akazingatia maadili ya kazi zake.
Hata hivyo,Bw.Francis ameipongeza ofisi ya ukaguzi wa hesabu za serikali ,C.A.G ikiongozwa na kiongozi wake Mahiri Profesa Musa Assad kwa kuendelea kutoa ripoti ya ukaguzi kwa wakati kila mwaka bila upendeleo wowote katika kusukuma gurudumu la Maendeleo kwa kuelekea Uchumi wa kati wa Tanzania ya viwanda.
Kuhusu changamoto zinazoikabili ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za serikali C.A.G hususan upungufu wa wafanyakazi Bw.Francis amesema ofisi yake ipo tayari kutatua tatizo hilo ambapo ameitaka ofisi ya C.A.G kufanya mchakato wa kuorodhesha idadi husika ya upungufu huo.
Katibu wa TUGHE Taifa Heri Mkunda amezungumzia juu ya Ushirikishwaji wa wafanyakazi katika bajeti ili kujenga dhana ya utawala bora .
Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi ofisi ya Taifa ya ukaguzi C.A.G Prof.Musa Assad amesema ofisi yake ina watumishi 957 huku kukiwa na upungufu wa watumishi zaidi ya hamsini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kustaafu,kufariki au kuhamishwa taasisi nyingine.
Kaulimbiu ya mkutano mkuu wa mwaka wa Baraza la Wafanyakazi ya ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ni Ukaguzi Shirikishi ,Uwazi na Uwajibikaji ni nguzo muhimu katika kufikia uchumi wa kati.