Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde amebainisha kuwa Rais Magufuli ni miongoni mwa Marais ambao walipokelewa kwa shangwe kubwa sana, wakati akiwasili kwenye hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa,
Naibu Waziri Mavunde amesema hayo jjijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Ubungo ya Kijani, ambayo imelenga kuelekea uchaguzi za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu hapa nchini 2020.
"Mimi nimetoka nje ya nchi jana (Namibia), ukitamka Magufuli nje ya mipaka ya Tanzania anapokelewa kwa shangwe kubwa sana, na ndiyo maana Afrika Kusini alipokelewa kwa shangwe kubwa kuliko Marais wote, ni uthibitisho kwamba Rais anafanya vizuri sana Afrika", amesema Mavunde.
"Nje ya mipaka ya Tanzania wanaona kazi nzuri iliyofanywa na Rais Magufuli, sisi watu ndani macho yetu yanapaswa kuona vizuri zaidi, nawashukuru zaidi Madiwani ambao mmeamua kumuunga mkono", ameongeza Mavunde
Mapema jana kiongozi huyo alizindua kampeni hiyo ya Ubungo ya kijani ikiwa kuelekea chaguzi mbalimbali nchini ambapo chama hicho kimelenga kurejesha baadhi ya maeneo ambayo yanaongozwa na vyama vya upinzani katika mkoa wa Dar es salaam.
Ubungo ya kijani, nilifikiri kupanda plants na majani kuiremba ubungo!
ReplyDelete