Waziri Lugola Atoa Miezi Miwili kwa Shirika la Uzalishaji Mali Jeshi la Magereza

Waziri Lugola Atoa Miezi Miwili kwa Shirika la Uzalishaji Mali Jeshi la Magereza
Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola ameiagiza bodi mpya ya Shirika la uzalishaji mali la Jeshi la Magereza nchini, ndani ya miezi miwili ihakikishe maeneo yote yaliyochini ya miliki ya Jeshi hilo yamepimwa na kuwa na hati miliki pamoja na nyaraka zote.

Sambamba na hilo bodi ihakikishe inakuja na mipango thabiti ya kuimarisha shirika hilo, ikiwa ni  pamoja na  Jeshi la Magereza linajitegemea kwa kila kitu bila kutegemea Serikali kuu.

Waziri  Kangi  Lugola umetoa maagizo hayo  Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa bodi ya Shirika la uzalishaji mali la jeshi la Magereza iliyoundwa kusimamia miradi yote iliyochini ya Shirika hilo ili iweze kuleta tija kwa Jeshi na jamii.

Amesema bodi hiyo  ihakikishe ndani ya miezi miwili kwa kushirikiana na wataalamu ndani ya Jeshi hilo maeneo yote yanayomilikiwa na jeshi la magereza yawe yemepimwa na kuwa na hati miliki halali, kwa sababu kumekuwa na migogoro mingi katika  maeneo hayo kwa sababu hayana hati miliki na kushindwa kuendelezwa.

“Niwaagize bodi mpya ndani ya miezi miwili muhakiki mnakuja na mpango mkakati wa kuhakikisha shirika hili linainuka kutoka hapa lilipo na kufikia kujitegemea kwa kila kitu bila kutegemea hata senti moja  kutoka serikali kuu”,

Ameitaka bodi hiyo kuhakikisha inatatua changamoto zote ambazo zinaikabili shirika hilo ambazo  zilikuwa zinasababisha shirika hilo kuto kuendelea na kuleta tija  kama malengo ya kuanzishwa kwake ikiwa ni pamoja na kupunguza msongamano wa mahabusu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad