Narendra Modi ameapishwa kuwa waziri mkuu wa India kuhudumu kwa muhula wa pili mfululizo kufuatia ushindi mkubwa wa chama chake katika chaguzi kuu za hivi karibuni zilizofanyika nchini humo.
Sherehe hiyo ya kuapishwa kwa Modi na Baraza lake la Mawaziri jipya ilifanyika katika eneo wazi mbele ya ikulu ya Rais ya Rashtrapati Bhawan iliyoko katika Raisina Hill katika mji mkuu wa India.