Waziri Mwakyembe Akerwa na Vyombo vya Habari vya nje Vinavyopotosha Kuhusu Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amevitaka vyombo ya habari vya Nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania kutangaza na kuandika habari za kweli ili kujitofautisha na vyombo vya Nje ya Bara hilo ambavyo upotosha na kubeza kwa makusudi mambo mazuri yanayotekelezwa na yaliyotekelezwa na Nchi za Afrika. 


Akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Mawasiliano Barani Afrika leo Ijumaa (Mei 24, 2019) Jijini Dar es Salaam, Dkt. Mwakyembe alisema vyombo vya Habari vya Afrika havina budi kuonyesha udhubuti kwa kuweka sera zinazoakisi maendeleo na kuyatangaza kwa Wananchi wake na wote waliopo nje ya Bara hilo. 


Dkt. Mwakyembe alisema sehemu kubwa ya maudhui ya Vyombo vya Habari vilivyopo nje ya Bara la Afrika vinavyoongozwa na Wakoloni waliowahi kutawala katika Bara la Afrika hawapendi kuona Nchi za Afrika zinapiga hatua za Maendeleo kwa wananchi wake na badala yake hupenda kuripoti na kutangaza mambo mabaya yanayohusu Afrika ikiwemo njaa, magonjwa, vurugu za kisiasa, vita n.k. 


Aidha Dkt. Mwakyembe alisema yapo mambo mazuri ya Maendeleo yanayofanyika katika Nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania ambayo zimepiga katika kipindi cha miaka minne imepiga hatua kubwa katika Maendeleo ya kiuchumi, na miundombinu, jambo ambalo baadhi ya vyombo vya habari vya Mataifa ya Nje ya Afrika yamekuwa hayapendi kuyatangaza, hivyo ni wajibu wa vyombo  vya habari kutumia majukwaa yao kutetea na kutangaza mafanikio hayo. 


“Wakati Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Kenneth Kaunda wa Zambia walipoamua kujenga Reli ya Tazara, walipingwa vikali sana Wakoloni waliotuwala na wengine waliita reli ile kuwa ni bamboo (mianzi) lakini ni taifa moja tu la Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China walitusaidia na leo hii reli ile ndiyo ndefu zaidi katika Bara la Afrika yenye urefu wa kilometa 1860” alisema Dkt. Mwakyembe. 


Kwa mujibu wa Waziri Mwakyembe alisema Maendeleo ya Bara la Afrika yatatetewa na kupiganiwa na Wafrika wenyewe, hivyo ni wajibu wa vyombo vya habari vya Bara hilo kujitokeza na kutetea Maendeleo hayo na kamwe haitatokea siku moja chombo cha habari cha BBC au CNN vikatangaza mafanikio hayo kwani hawapendi kuona Mataifa waliyoyatawala yakifikia hatua kubwa za kimaendeleo.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Karl Marx alisema media ni tools zinazotumiwa na bourgeoisies ili influence interest zao kwa manufaa yao.

    ReplyDelete
  2. Dawa yake ni wewe Mr mwakyembe na wizara yako ya Habari na watanzania, kuweka comments ili kukanusha upotoshaji huo. Lakini inashangaza wala hakuna comments kuchallenge taarifa za uongo. Mataifa mengine watu wapo active kutoa comments. Mr kauli hii huenda itakomea masikioni mwa watanzania tu. Lakini ukicomment kwenye vyombo vya kimataifa huenda italeta umaana zaidi. Asante.

    ReplyDelete
  3. Pia usisahau ngos hujipatia funds kwa kutoa picha duni za Africa kwenye media zilizoambatana na ujumbe wa kusikitisha juu ya bara hii ili kuhimiza watazamaji wa media kutoa mchango wa kifedha. Daima wao hulenga watu wenye njaa, mazingira duni ya kifukara yenye ukosefu wa maji, nyumba bora, mavazi, magonjwa, miundo mbinu duni. Kama wataweka picha safi ya Africa huenda mashirika hayo yatakosa support toka kwa wafadhili wao. Hivyo, kama bado tuna nia ya kupokea misaada toka ngos, picha chafu za Africa kwenye media za ughaibuni ni vigumu kuzitokomeza.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad