Wizara ya Michezo Yaona Jitihada za Samatta Yamwandalia Zawadi

Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, ametoa pongezi kwa nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta baada ya kuisaidia timu yake ya KRC Genk kuibuka mabingwa wa Ubelgiji.

Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa Samatta amefanya jambo kubwa kwa kuzingatia Ubelgiji ni moja ya mataifa makubwa tena yanayofanya vizuri kwenye mchezo wa soka duniani.

''Samatta amefanikiwa kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania, ni shujaa ambaye mchango wake ni mkubwa na tunajaribu kuona ni vipi Samatta anaweza kuwa Balozi wa vivutio vyetu vya utalii, Sanaa na Michezo'', amesema.

Mbwana Samatta ambeye ni mchezaji wa zamani wa Simba, TP Mazembe na mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2016, mpaka sasa ni kinara wa mabao kwenye ligi kuu ya Ubelgiji akiwa amefunga magoli 20.

Samatta alijiunga na Genk mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ambapo mwaka huo pia alishinda tuzo ya mchezaji bora wa ndani Afrika baada ya kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad