Zari Kuitikisa Mbagala Kesho


Mambo ni faya! Wakati saga lake na mzazi mwenzake ambaye ni staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ halijapoa, mwanamama huyo anatarajia kuitikisa Mitaa Mbagala jijini Dar.  Ijumaa linafahamu kuwa Zari ambaye ni Balozi wa Pampers za Softcare anatua Bongo leo akitokea nyumbani kwake, Afrika Kusini kwa ajili ya shughuli za kijamii.

Katika mahojiano na Gazeti la Ijumaa juu ya ujio wa Zari ambaye ni gumzo kutokana na ugomvi wake na Diamond au Mondi, mmoja wa wawakilishi wa Kampuni ya Softcare aliyejitambulisha kwa jina la Lucy alisema kuwa, waliamua kumchagua Zari kwa sababu ni mtu ambaye amejipatia umaarufu nchi mbalimbali.

“Unajua tuliona kabisa Zari ana mashabiki wengi na sisi nia yetu ni kwamba bidhaa zetu zisambae sehemu mbalimbali siyo Tanzania tu maana tunauza bidhaa zetu nje ya nchi pia,” alisema Lucy.


Mwakilishi huyo aliendelea kusema kuwa, Zari atatua Ijumaa (leo) ambapo atakuwa na walinzi watakaomsubiria uwanja wa ndege ambao watamsindikiza hadi hotelini kisha kesho yake (Jumamosi) ataamkia katika Hospitali ya Mbagala akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar (Felix Lyaniva).

“Kesho wakazi wa Mbagala wakae tayari maana Zari atakuwa kwenye wodi ya kina mama na watoto ambapo atatoa misaada mbalimbali pale,” alisema Lucy. Zari aliyezaa watoto wawili na Mondi anatua Bongo katika kipindi ambacho kuna vuguvugu kubwa juu ya ugomvi wake na staa huyo wa Bongo Fleva.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad