Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameitaka Serikali kuhakikisha inatoa kwa haraka vitambulisho vya taifa ili kuondokana na usumbufu wanaopata wananchi wanaoishi maeneo ya mpakani ambao wamekuwa wakisumbuliwa kuhusiana na suala la uraia.
Zitto Kabwe ametoa rai hiyo Bungeni jijini Dodoma wakati wa maswali na majibu, ambapo aliihoji Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi juu ya tatizo hilo, "bado kuna unyanyasaji wa wananchi kuhusu uraia, kwanini Serikali isitoe vitambulisho haraka", amehohi Zitto.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema kuwa, "kuhusu unyanyasaji wa wananchi tulifanyia kazi, nimpongeze kwa rai yake, aliyosema ni rai ya Serikali kufikia malengo wananchi wapate vitambulisho".
Kwa sasa Bunge linaendelea jijini Dodoma ambapo Mawaziri mbalimbali wameendelea kuwasilisha makadirio ya Bajeti ya Wizara yao.