Akiona hatumsaidii anatuondoa, mniombee nisitoke mapema” Mkurugenzi TIC

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimewataka wakazi wa Makete waishio DSMSM kupitia umoja wao Chama cha Maendeleo Makete (MDA) kuanzisha Kampuni ya Uwekezaji Makete (Makete Investment Company) kwa lengo la kusimamia uanzishaji wa miradi ya uwekezaji sambamba na kuanzisha Mfuko wa Maendeleo wa Makete (Makete Development Fund) utakaosaidia kutafuta na kubuni vyanzo vya fedha zaidi zitakazosaidia kutekeleza miradi mbalimbali ili kuongeza tija ya MDA na kushawishi Wanamakete kuwekeza zaidi kwenye fursa zinazopatikana Wilayani humo na hatimae kukuza uchumi wa Taifa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffrey Mwambe ameyasema hayo katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Chama cha Maendeleo Makete (MDA) uliofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo alisema pamoja na Chama kuwa na lengo la ushirika pia kinatakiwa kuongeza hamasa/nguvu katika eneo la kuwekeza kwa maendedeleo ya Makete na Taifa kwa ujumla. Jambo hili likifanikiwa litakuwa na tija zaidi kwa Wanamakete kutokana na fursa nyingi zilizomo ndani ya Wilaya hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad