Alikiba na Mbwana Samatta apatoshi leo uwanjani

Leo Jumapili hutakiwi kukosa pale Uwanja wa Taifa kwani mastaa Mbwana Samatta na Ally Saleh Kiba na timu zao watakuwa wakionyesha umwamba katika mchezo maalum uliopewa jina la Nifuate huku kila upande ukitamba kuwa lazima ushinde. 


Mchezo huo ni maalumu, umeratibiwa na Samakiba Foundation kwa lengo la kuhakikisha wanarudisha shukrani zao kwa jamii yote hususani ile yenye mahitaji maalum na mechi ya kesho itakuwa ya pili kwani mwaka jana ilichezwa kwa mara ya kwanza. 


Benchi la Timu Samatta litakuwa likiongozwa na Kocha Ammy Ninje ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF wakati Timu Kiba nayo imeleta Kocha kutoka Colombia aitwaye, Edwardo Tamiyo. Alikiba alisema; 


“Nimemchukua kocha wa kigeni ili kuleta utofauti kidogo na kubwa zaidi ni kuongeza chachu na ladha ya mchezo huu ambao awamu hii mimi nitakuwa timu mwenyeji. 


Wakati Kiba akimuweka wazi kocha wake, Samatta yeye alifanya siri, lakini Championi Jumamosi liliweza kupata taarifa kutoka kwa mwakilishi wa mmoja ya wadhamini wa mchezo huo ambaye hakutaka kutajwa ambapo alisema: “Timu Samatta itakuwa chini ya Ammy Ninje.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad