Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umetoa tahadhari nyingine ya shambulio la kigaidi nchini humo
Kulingana na tahadhari hiyo iliochapishwa katika ukurasa rasmi wa mtandao wa kijamii wa balozi hiyo, kuna uvumi wa mipango ya mashambulizi katika maeneo yanayopendwa sana na raia wa kigeni katika Afrika Mashariki ikiwemo Uganda.
Ubalozi huo umesema kuwa ijapokuwa hauna ushahidi wa kutosha kuhusu tishio hilo ama habari kuhusu wakati ambapo mashambulizi hayo yatafanyika umewaonya wakaazi kuchukua tahadhari.
"Ubalozi hauna ushahidi wa moja kwa moja wa tishio hilo ama taarifa za muda gani mashambulizi yatatokea, hata hivyo unawaonya wananchi kuchukua tahadhari."
'Jeshi la polisi lilipata fununu za tishio la ugaidi kabla Ubalozi wa Marekani'
Makonda: Hakuna tishio Dar es Salaam
Je, Kenya tayari kuna noti mpya bandia?
Umewataka raia kuwa macho wakati wowote katika maeneo wanayozuru, kutahadhari dhidi ya makundi ya watu wengi mbali kufuatilia habari zinazochipuka mara kwa mara .
Aidha umewataka raia kuwa macho katika maeneo yanayopendelewa sana na watalii hususan wale wa mataifa ya magharibi.
Tahadhari hiyo inajiri siku moja tu baada ya ubalozi huo kutoa tahadhari nchini Tanzania ambayo imewatakaa wakaazi kuchukua tahadhari hususan wale waliopo katika eneo la Masaki.
Eneo hilo lililopo kwenye rasi ya Msasani ni moja ya maeneo ya makazi ya kigahari zaidi jijini humo
Tahadhari hiyo ilibainisha kuwa, maeneo yanayolengwa ni mahoteli na migahawa ambayo hutembelewa na watalii ikiwemo eneo maarufu la maduka ya Slipway.
Tutaendelea kukujuza zaidi kadri tutakavyokuwa tunapokea taarifa juu ya tahadhari hiyo.
Baada ya Tanzania Ubalozi wa Marekani Watoa Tahadhari ya Shambulio Uganda
0
June 20, 2019
Tags