Baba na mwanaye wa miaka miwili wafariki wakivuka mto

Picha ya kusikitisha ya mhamiaji wa Salvador na binti yake mwenye umri wa miaka miwili ambao walifariki wakati wakijaribu kuvuka mto Rio Grande kutoka Mexico kwenda Marekani imezua majonzi na hasira, na kudhihirisha hatari zinazowakabili wanaotafuta hifadhi.

Oscar Martinez Ramirez mwenye umri wa miaka 25 pamoja na mkewe mwenye umri wa miaka 21 wakiwa na binti yao walifanya uamuzi hatari wa kuvuka mto kutoka Mexico hadi Marekani siku ya Jumapili alasiri, kwa mujibu wa ripoti ya mahakama ya Mexico.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad