Baraza la Kijeshi Sudan Lasema Liko Tayari Kuzungumza Tena

Mkuu wa baraza la kijeshi la Sudan amesema baraza hilo liko tayari kwa majadiliano kuhusu mustakabali wa taifa hilo, siku moja baada ya kuyasimamisha.

Amesema wako tayari kuzungumza kwa maslahi ya kitaifa na mapinduzi.
Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametoa matamshi hayo katika ujumbe wa sherehe ya Eid al- Fatr, siku moja baada ya kutangaza kwamba baraza la mpito MTC limefuta makubaliano yote na muungano wa waandamanaji na makundi ya upinzani, na badala yake walikuwa wanakwenda kwenye uchaguzi wa taifa katika kipindi cha miezi tisa.

"Sisi katika Baraza la Kijeshi tunafungua mikono yetu kwa majadiliano bila vikwazo vyovyote zaidi ya maslahi ya kitaifa ya kuendelea kujenga mamlaka halali inayoakisi malengo ya mapinduzi ya Sudan kwa kila njia," alisema Burhan katika hotuba kupitiatelevisheni ya taifa.

Idadi ya vifo yafika 60
Kamati kuu ya madaktari wa Sudan, imesema idadi ya waliouawa katika ukandamizaji wa kijeshi imepanda na kufikia watu 60, na kwamba zaidi ya 300 walijeruhiwa, ingawa imekuwa vigumu kubainisha hasa idadi ya waliojeruhiwa kwa sababu baraza la kijeshi limezima mawasiliano ya intaneti katika maeneo mengi ya nchi.

Idadi ya awali ya waliouawa ilikuwa 40, lakini kamati ya madaktari inasema vikosi vya usalama viliuwa watu wasiopungua 10 mapema Jumatano katika mji mkuu Khartoum na mji wake pacha wa Omdurman
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad