Bashungwa amjia juu Peter Msigwa 'athibitishe kama korosho ya Tanzania imeoza'

Baada ya Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema) baada ya kudai korosho ya Tanzania imeoza, Waziri  wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashugwa amemjia juu Mbunge huyo.

“Serikali imekuwa ikisema inamjali mtu mnyonge, kimsingi mtu mnyonge kwa Tanzania ni mkulima, kwa bahati mbaya Serikali imewaletea adha na kuwavuruga wakulima wa korosho, sasa mmeanza kuwavuruga wakulima wa pamba,” alisema Msigwa akichangia mjadala wa Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2019.

Wakati Msigwa akiendelea kuchangia, Bashungwa alimkatisha kwa kutaka kumpa taarifa na Naibu Spika Dk. Tulia Ackson alimruhusu.

Bashungwa alisema anayosema Msigwa si kweli na Serikali haijawavuruga wakulima wa zao la korosho na korosho ya Tanzania ipo vizuri na ina ubora wa hali ya juu.

“Serikali haijavuruga wakulima wa korosho na korosho yetu bado ni bora na tunataka kuiambia dunia kwamba korosho ya Tanzania ni bora."

“Wewe ndio unavuruga wakulima na sio Serikali, tutangulize uzalendo kwanza,” alisema Bashungwa.

Msigwa aliendelea kwa kudai taarifa ya Bashungwa haipokei na kwamba wamepeleka bei za kinyonyaji na uporaji kwa wakulima wa korosho.

“Taarifa yake siipokei, hizi ni bei za kinyonyaji, hizi korosho bora mkazichome tu kwani zinaoza na  zitaharibu soko la baadae, hizi zichomeni moto,” alisema.

Kutokana na maelezo hayo, Bashungwa alisimama tena kwa kutumia kanuni ya 63 (4) na alimtaka Msigwa kuthibitisha kauli yake kwamba korosho zimeoza.

“Amesema korosho ya wakulima wetu imeoza na mimi nimetoka huko, korosho ni bora, athibitishe kama imeoza kweli kama haijaoza  achukuliwe hatua,” alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad