Bilionea Mdogo Duniani Azidi Kutanua wigo


Bilionea mdogo zaidi aliyetajwa katika jarida la Forbes , Kylie Jenner, azidi kutanua wigo katika biashara zake anazozifanya.

Kylie ambaye ana umri wa miaka 21 , amefungua alama ya biashara yake mpya iitwayo Kylie Booze, ambayo itakuwa na bidhaa za vinywaji kama mvinyo wa wine, pombe, bia, vinywaji visivyo na vilevi pamoja na vinywaji vya kuongeza nguvu.

Mwezi mmoja uliopita alifungua alama ya biashara yake iitwayo "Kylie baby" ambayo inazalisha bidhaa zote za watoto, pia ana biashara yake ya "Kylie Hair" ambayo inadili na maswala ya nywele za kina dada.

Pia ana biashara yake ya vipodozi iliyomfanya kuwa bilionea iitwayo "Kylie Cosmetics"
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad