Ziara hiyo iliyofanyika Ijumaa Juni 21, 2019 pia iliwahusisha wajumbe wa Kamati ya Maudhui ya TCRA.
Akizungumzia nia ya ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James M. Kilaba alisema, Mamlaka kama Mdhibiti na Msimamizi wa Mawasiliano nchini, imeona ni vema kutembelea taasisi hizo mbili kwani kuna mambo ya msingi yanayofanywa na taassi hizo yanahusiana moja kwa moja na huduma zinazotolewa na TCRA.
“Lengo la ujio wetu hapa Terminal III nikuangalia katika hatua hizi ambazo ujenzi umekamilika ni mahitaji yapi ambayo bado ili sisi tuongeze ushiriki wetu ili kuyakamilisha hususan katika mifumo ya mawasiliano.” Alsiema Mhandisi Kilaba.
Alisema wakiwa hapo TBIII wamepata fursa ya kuulizia hali ya mawasiliano kama imekamilika ambapo watoa huduma, TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo, Zantel, Halotel na hata Internet kama wako tayari.
“Huduma hizi ni muhimu sana na zinatakiwa ziwe kwenye maeneo kama haya kwa sababu zinawezesha hata kufanya utalii kuwa rahisi, mgei anapoingia hapa na anataka kwenda eneo Fulani la utalii lazima awasiliane, lakini pia TCRA inatoa masafa kwa ajili ya kuongozea ndege zinapotua na kuruka na lengo hasa ni kuhakikisha hakuna muingiliano katika huduma hizo." Alibainisha Mkurugenzi huyo Mkuu wa TCRA.
"Kuja kwetu kumetupa fursa ya kujifunza mengi kama ambavyo watanzania wanaweza kushuhudia kuwa kiwanja hiki ni kizuri, kinapendeza na mawasiliano yapo yanaendelea kukamilishwa na tumejionea hata Wifi point ipo.” Alifafanua Mhandisi Kilaba.
Aidha kuhusu Maktaba mya ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhandisi Kilaba alisema, Maktaba hiyo inatumia huduma za TCRA kwani moja ya huduma zitolewazo ni pamoja na Maktaba mtandao (e-library) na hili ni jambo jema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Dkt.Jones Killimbe alisema, ziara hiyo imekuwa ni ya mafanikio makubwa kwani imewezesha timu nzima ya TCRA, Wajumbe wa Bodi, Menejimenti, Wajumbe wa Kamati zinazosaidia kutekeleza majukumu kwenye mamlaka kwa pamoja wameelimika sana.
“Kiwanja hiki katika lugha ambayo ningeiazima ni flagship project….ni mradi wa kimkakati wa taifa hili... nikisema kimkakati ni kwasababu mojawapo ya masuala ya kiuchumi ya nchi yetu ni utalii, na nadhani huu utakuwa mlango mkubwa sio dirisha…utakuwa mlango mkubwa wa utalii na mchango wa utalii kwenye uchumi wetu utaongezeka sana.” Alisema Dkt. Killimbe.
Ziara hiyo imewezesha wajumbe kupata maelezo ya kina ya kukamilika kwa huduma mbalimbali kwenye jengo la TBIII hali kadhalika kwenye maktaba ya ksiasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaa,