CAG Atoa Neno Kukaguliwa na Bunge
0
June 19, 2019
Profesa Mussa Assad ambaye Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amesema siyo jambo jipya ofisi yake kufanyiwa ukaguzi.
Prof. Assad amesema hatua hiyo hufanyika kila mwaka na taarifa kuwasilishwa Kamati ya Bunge la Hesabu za Serikali (PAC).
"Tunakaguliwa kila mwaka na mkaguzi wetu kama kawaida atateuliwa na PAC ya Bunge atafanya kazi yake, akimaliza atatoa ripoti na kuitazama sisi na kusainiwa na audit committee halafu hesabu hizo zitapelekwa kwa mwenyekiti wa PAC ili kusoma bungeni," Profesa Assad alisema hayo wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha Azam.
“Hayo ni mambo ya kawaida kabisa katika utendaji wa taasisi yetu na siyo jambo jipya, ni matakwa ya kisheria,” alisema Profesa Assad.
Mei 16, 2019, Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alitoa taarifa bungeni kwamba kwa mujibu wa sheria ya ukaguzi wa umma, hesabu za ofisi ya CAG zinakaguliwa na Bunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).
Tags