China Yalipiza Kisasi kwa Marekani..Yaanza kushughulia Makampuni Kutoa Huko

Wizara ya biashara ya China leo imetangaza kuwa itaanzisha orodha ya makampuni yasiyoaminika, ikiwa ni pamoja na makampuni yasiyofuata kanuni za kisoko, kukiuka mikataba, kukataa kutoa bidhaa kwa China bila ya malengo ya kibiashara, na kuathiri maslahi halali ya makampuni ya China. 


Hii ni hatua ya kulipiza kisasi kwa Marekani, ambayo imeweka vikwazo dhidi ya makampuni kadhaa ya China bila ya ushahidi wa makosa. China imefafanua kuwa haipendi na wala haiogopi vita vya kibiashara kati yake na Marekani. 


Katika zaidi ya mwaka mmoja uliopita, China imefanya duru 11 za mazungumzo na Marekani kuhusu suala la biashara. Wakati huohuo Marekani imeongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za China mara kadhaa, na kuweka vikwazo dhidi ya baadhi ya makampuni ya China. 


Hali hii imeilazimisha China itoe majibu thabiti. Kuanzia tarehe mosi Juni, China itaongeza ushuru wa bidhaa kutoka Marekani kwa asilimia 25, 20 na 10, na kuanzisha orodha ya makampuni yasiyoaminika. Aidha China inafikiria kuuzuia utoaji wa udongo adimu kwa Marekani. 


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad