FAMILIA ya aliyekuwa gwiji wa sanaa nchini, Kapteni Jonh Komba, inatarajia kuzindua taasisi ya kumbukumbu ya kuenzi sanaa yake na kuanzisha bendi ya muziki itakayoimba sauti ya Kapteni Komba, familia hiyo imeipa taasisi hiyo jina la The Capten Komba Arts Memorial Foundation.
Kapteni Komba ambaye aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi, alifariki siku ya Jumamosi Februari 28, 2015 katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na vyombo vya habari kwa niaba ya familia na taasisi hiyo, Salome Komba, mjane wa Kapteni Komba ambaye pia ndio katibu wa taasisi hiyo amesema, uzinduzi wa taasisi hiyo utakwenda sambamba za uanzishwaji wa bendi ya muziki itakayoenzi sanaa ya Kapteni Komba.
Taasisi hiyo itazinduliwa Julai 6, 2019 katika Ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho ya Taifa, Kijitonyama, Dar es Salaam.
”Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Dk. Bashiru Ali na kuhudhuriwa na wabunge mbalimbali pia viongozi wa serikali pamoja na wasanii,” amesema Mama Solome.
Amesema kuwa, taasisi hiyo imejenga makumbusho ya kumuenzi Kapteni Komba ambapo ujenzi wake ulizinduliwa na Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Februari 28, 2018.
Aidha, familia hiyo imemuombea msamaha Captain Komba kama kuna mtu alimkwaza enzi za uhai wake katika kazi yake za sanaa na siasa pamoja na maisha ya kawaida.
Familia ya Captain Komba Yaamua Sasa Kuzindua Taasisi ya Kumbukumbu Kumuenzi
0
June 10, 2019
Tags