Gwajima Akutana na Rais Magufuli Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amekutana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephati Gwajima, Ikulu Jijini Dar es salaam.


Akizungumza mara baada ya kutoka kwenye mazungumzo na Rais Magufuli, Askofu Gwajima amempongeza Rais Magufuli kwa kuazimia kutekeleza mradi wa umeme wa Striglers Gorge.

Askofu Gwajima amesema, "kwanza lazima tuelewe ili ule chips yai lazima uvunje baadhi ya mayai, namshukuru Rais juhudi zake za Stiglers George mahala ambapo tutazalisha umeme mwingi kuliko tuliowahi kuzalisha hapo zamani, kama unavyojua watu wengi wa Magharibi wanasema eneo hilo ni la mazingira lakini ukweli wenyewe ni siasa tu za kimataifa".

Hivi karibuni ilizuka taharuki kufuatia kusambaa kwa kipande cha video ambayo ilidaiwa kumuonesha mtu aliyefanana na kiongozi huyo wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Gwajima akishiriki mapenzi na msichana.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad