Hawa Hapa Wadaiwa Kumuua Mtoto Wao ili Kunusuru Ndoa Yao

Stephen Kamau Kariuki na mke wake Mildred Musya wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Sheila Nyaga jana Jumatatu baada ya kukamatwa na Polisi siku ya Jumapili

Wanandoa hao wanaoishi huko Murang'a walikamatwa wakidaiwa kumuua mtoto wao baada ya mwili wa mtoto wao huyo mwenye miaka miwili kupatikana katika mto Mathioya baada ya kupotea kwa siku nne

Kwa mujibu wa Mpelelezi wa Polisi, Ignatius Ewoi, mtoto huyo, Sibly Matsista alipotea Mei 28, 2019 alipoenda kuchota maji na mama yake lakini inadaiwa wanandoa hao walimuua na kuzidanganya Mamlaka kuwa kapotea

Inadaiwa Mwanamke huyo amemuua mtoto huyo kutokana na ugomvi ulipo baina yake na familia ya Mumewe ambapo familia hiyo imekuwa ikikwaruzana naye juu ya mtoto huyo na kutokana na yeye kuolewa akiwa na watoto wawili tayari

Mmoja wa Wanakijiji,  Lucy Wanjiku alisema si mara ya kwanza Mwanamke huyo kujaribu kumuua mtoto huyo kwani siku si nyingi alijaribu kumuua kwa kumuwekea sumu lakini hakufanikiwa 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad