Hiki Ndicho Kinachoendelea Katika Mzozo Kati ya Iran na Marekani


Kama umekuwa ukifuatilia mzozo wa Ghuba bila shaka umesikia kuhusu mvutano uliopo kati Iran na Marekani.

Rais Donald Trump alikuwa amebakisha dakika 10 kuishambulia kijeshi taifa hilo na kwamba Marekani ilikuwa imesema itatuma wanajeshi 1000 Mashariki ya Kati kufuatia kile ilichotaja kuwa''uchokozi'' wa vikosi vya Iran.


Marekani iliilaumu Iran kwa kuzishambulia meli ya mbili za mafuta za Japan katika GhubaOman - jambo ambalo Irana imekanusha.

Pia kuna hali ya taharuki kwasababu Iran imesema itakiuka mkataba wa Kimataifa wa nyuklia uliofikiwa mwaka 2015.

Mvutano huu ulifikaja hapa?

Haki miliki ya pichaEPA
Mfumo wa kuzalisha nguvu za umeme kwa kutumia nguvu za nyuklia hutumiwa na mataifa mengi, Iraniliadhibiwa na kuwekewa vikwazo vya kufanya biashara na nataifa mengine baada ya kushukiwa huenda mpango wake wa nyuklia unatumiwa kuunda bomu kisiri.

Iran inasisitiza kuwa shughuli zake za kinyuklia ni salama- jamii ya kimataifa haijafanikiwa kuthibitisha kama hilo ni kweli au la.

Urusi kuwafungulia nyangumi kutoka 'jela'
Kati ya mwaka 2012 na 2016, Iran ilipoteza takriban pauni bilioni 118 baada ya kuwekewa vikwazo.

Mwaka 2015 Iran ilikubali kuweka saini mkataba wa kimataifa wa wa nyuklia ili Iruhusiwetena kufanya biashara na mataifa mengine duniani.

Lakini rais Donald Trump alijiondoa katika mkataba huo mwaka 2018 na kuiwekea tena vikwazo Iran.

Vikwazo hivyo ni vipi?
Ununuzi wa noti za Marekani unaofanywa na Iran.
Biashara ya dhahabu na vyuma vingine
Graphite, aluminium, chuma, mkaa na programu zinazotumiwa katika sekta ya viwanda
Ubadilishanaji wa fedha unaohusishwa na sarafu ya Iran
Vitendo vinavyohusishwa na ulipaji madeni ya Iran
Sekta ya magari ya Iran
Vikwazo hivyo viliathiri uchumi wa nchi hiyo- kwa sababu ililenga sekta yake kuu wa mafuta, na benki.

Iran ilijibu hatua hiyo kwa kukiuka baadhi ya vipengee katika mkataba wa kimataifa wa nyuklia, na kuilaumu Uingereza na mataifa mengine ya Ulaya kwa kushindwa kutekeleza ahadi zao za kulinda uchumi wa Iran dhidi ya vikwazo vya Marekani .

Lakini tatizo sio kuhusiana na mzozo wa nuklia pekee.

Siku wa Alhamisi Iran ilidungua ndege ya kijasusi ya Marekani isiyo na rubani kwa matai ya kuingia kwenye anga lake bila idhini- madai amabayo Marekani inapinga.

Rais Trump aliripotiwa kuidhinisha mashambulio ya kijeshi dhidi ya Iran kwa kuidungua ndege yake lakini inadaiwa baadae alibadili msimamo huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad