Hivi Kwanini Ukiacha KAZI na Ujiajiri Jamii Haikuelewi Kabisa..



Watu wengi wanaamini katika kuajiriwa kuliko kujiajiri, wazazi wengi wanatumia pesa nyingi kuwatafutia vijana wao kazi, lakini ni wachache wanaoweza kuwapa vijana wao mitaji kwa ajili ya biashara.

Jamii Inaamini ukiajiriwa umeula bila kujali kipato, ndio maana mwajiriwa anabebeshwa mzigo mzito sana na familia yake, mfano kukiwa na vijana wawili moja mwajiriwa mwengine aliyejiajiri, kila shida ya familia huibeba mwajiriwa hata kama aliyejiajiri amemzidi kipato.

Sasa mwajiriwa akitaka kuacha kazi na kujiajiri jamii humshangaa na sana na kumuona kama mtu aliyepotoka, jamii Inaamini mtu mwenye ajira ana uhakika wa maisha, ukitaka kuthibitisha hilo waambie ndugu zako unataka kuacha kazi uone wanavyokushauri.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad