Huyu Hapa Dereva wa Basi Wakipekee, Ukisafiri Nae Hutotamani Ufike

MWAKA 1992, ulikuwa ndio mwaka wangu uliokuwa na furaha kubwa wakati nilipouona mlima Kilimanjaro kutoka juu angani.

Tukiwa katika anga la Sudan, rubani wetu , ndani ya ndege ya Shirika la Ndege la Uholanzi (KLM) amesema:

“ Abiria wapenda, tunakaribia anga la Afrika Mashariki.Tunazungumza na serikali ya Tanzania kuona uwezekano wa kupita karibu na Mlima Kilimanjaro ili muuone mlima mkubwa katika tropiki wenye barafu.”


Mimi Mtanzania nilifurahi sana, kwani sijawahi kuuona mlima huo zaidi ninapokuwa na kwenda Arusha kupitia Moshi.


Si mimi tu ilionekana kila mtu alikuwa na hamu ya kujua nini kinaendelea.


Tukiwa ndani ya anga la Kenya, rubani yule alisikika tena akisema kwamba kutokana na hali ya hewa kuwa nzuri, tumepata ruksa ya kupita karibu sana na mlima huo ambao utakuwa upande wa kulia wa ndege.


Aidha amesema anashuka kidogo na kuilaza upande ndege ili abiria waweze kushuhudia uzuri wa mlima huo.

Rubani wa KLM mpaka leo namkumbuka, alielezea uzuri wa mlima huo na kweli anga lilikuwa la samawati na tuliona barafu ilivyojitengeneza, ikanikumbusha picha ya anga inayotumika katika atlas za zamani, hakika nilifurahi sana.


Nimekaa na kutembea sana toka mwaka huo, lakini sikuweza kupata aina ya rubani huyo mpaka niliposafiri hivi karibuni kwenda Dodoma kwa kutumia basi la ABC lenye namba za usajili T 893DJN na kukutana na dereva wa basi ambaye alinisaidia kufanya utalii wa ndani.


Alianza safari vyema pale Ubungo na baada ya utambulisho uliofanywa na kondakta wa basi ambaye alikuwa mdada, kwamba dereva wetu ni nani, tukiwa tupanda vilima vya kuelekea Kimara, alitukumbusha kuomba na kuiombea safari iwe salama hasa kwa siku hiyo ambayo kulikuwa na manyunyu njia nzima.


Alitusalimu kwanza kabla ya kuomba kwa pamoja na kisha kusema kila mtu aombe kwa dini yake tufike salama katika safari hiyo.


Nikasema leo nimekutana na mtu mwenye hofu ya Mungu na anayetaka wote tumuombe Mungu kufika salama kwa sababu tumo katika chombo.


Alitutaka tumuombe Mungu kufika salama tuendako ili tukatekeleze majukumu yanayotupeleka huko.


Alitueleza kwamba mwendo utapungua zaidi siku hiyo kuliko ule uliowekwa na serikali wa kilomita 80 kwa saa kutokana na hali ya hewa na mvua kubwa iliyokuwa inanyesha na kutueleza makisio ya muda wa kufika Dodoma.


Pamoja na kueleza safari itakuaje akaeleza maeneo ambayo kutakuwa na mapumziko mafupi kwa ajili ya kunyoosha miguu na kujipatia huduma mbalimbali ambazo katika basi hazipo, kama maliwato.


Mimi nilimpenda dereva ambaye anakueleza mapema vituo vya mapumziko na pia kueleza taarifa mbalimbali ambazo zinamhusu msafiri ili kujua haki zake na kwamba kukiwa na shida yeye na kondakta wake wapo tayari kusaidia.


Msaada mkubwa kutoka kwa dereva huyo, aliyejitambulisha kwa jina la Gabriel Balenga, ni kule kutoa maelezo ya maeneo mbalimbali katika njia ya Dar es salaam hadi Dodoma kwa kutumia kipaza sauti chake na kutufahamisha fursa mbalimbali zilizopo katika njia hiyo.


Wakati tunavuka mpaka wa Dar es Salaam kuingia Pwani maeneo ya Kibaha, Kiluvia alisema, “ndugu abiria kwa sasa tumemaliza mkoa Dar es Salaam na tumeingia mkoa wa Pwani. Katika dakika kumi zijazo tutaingia katika kituo kipya cha mabasi yanayokwenda Bara, Kibaha. Tutafanyiwa ukaguzi wa kawaida kabla ya kuendelea na safari yetu.”


Dereva huyu aliendelea kutueleza manufaa mbalimbali ya kituo hicho na tuliondoka hapo na kuendelea na safari. Maeneo ya Chalinze akazungumzia eneo la viwanda na fursa zake kabla ya kuingia mkoa wa Morogoro na kutueleza mambo mbalimbali ya Morogoro kasoro bahari.


Tulisimama kwa dakika kumi eneo la kunyoosha miguu kabla ya kuingia katika stendi ya Msamvu na kuendelea na safari kuelekea Dodoma.


Pamoja na taarifa mbalimbali tulipoingia maeneo ya Dakawa, alikuwa na jambo kubwa sana la kueleza.


Alizungumzia eneo la Dakawa, akazungumzia uongozi na ubora wa uongozi na kisha akatueleza kwamba tunakaribia eneo ambalo Waziri Mkuu wa tatu wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine alikufa mwaka 1984 alipopata ajali ya gari akitokea Bungeni Dodoma.


Huwezi kuamini takwimu alizotoa dereva huyu ambaye amezaliwa Agosti 28, 1976 zilikuwa sahihi mno kama vile kipindi kifo kinatokea alikuwa kijana mkubwa.


Alizungumzia vita dhidi ya rushwa na magendo iliyofanywa na Waziri Mkuu huyo na mwishoni akataka tuwaombee viongozi wetu.


Alipunguza sana mwendo wa gari katika eneo hilo akitaka wananchi , abiria kuona mnara uliopo mkono wa kulia ukiwa unatokea Dar es Salaam mahali ambapo ajali ilikuwa imetokea.


Kwa dereva huyu ambaye alikuwa na elimu kubwa ya njia yake, matukio ya njiani maeneo yenye biashara mbalimbali kubwa ambazo zinaweza kuwa fursa kwa abiria wake, ni aina ya dereve ambaye nimemuona Ulaya pekee nilipokuwa natembea katika teksi ya mjini London, yule dereva aligundua mimi mgeni na akawa ananiambia historia kidogo ya maeneo ambayo tulikuwa tunapita.


Wakati tunatoka Dumila alituambia tena kwamba sasa tunaanza kupanda taratibu kuelekea uwanda wa juu kuelekea Dodoma na kuwa tutashika mwendo kidogo kwa kuwa kumepambazuka.


Sijawahi kupata katika maisha yangu ya kusafiri hapa nchini kukutana na dereva ambaye anatumia usasa wa gari lake na vifaa vya gari vilivyowekwa kwa ajili ya kuwasiliana na wateja wake, tena akiwahabarisha mambo mbalimbali ya barabarani na kuwaweka katika raha.


Gabriel ambaye amezaliwa katika mkoa wa Tanga maeneo ya Muheza kwenye kijiji cha Kicheba alimaliza shule ya msingi Kicheba mwaka 1994 na hakubahatika kuendelea na shule ya sekondari kutokana na wazazi wake kutojiweza kiuchumi.


Shule aliyokuwa anasoma kwa sababu ambazo zinaeleweka serikalini kuanzia mwaka 1992 hadi 1994 haikuweza kufaulisha hata mtoto mmoja. Ilikuwa inazunguka katika


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad