ICC mbioni kusoma hukumu ya Bosco Ntaganda 'Terminator'

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) ya The Hague nchini Uholanzi Inatarajiwa kutoa hukumu ya aliyekua mbabe wa kivita nchini DR Congo, Bosco Ntaganda.

Ntaganda, maarufu kama 'Terminator' anashikiliwa na Mahakama hiyo tangu 2013 kwa makosa ya Uhalifu wa Kivita na Uhalifu dhidi ya binadamu.

Kati ya mwaka 2002-2003 vikosi vilivyokua vikiongozwa na Boscoi Ntaganda vilihusika kuajiri askari watoto, kufanya mauaji na ubakaji katika maeneo ya Ituri, Kaskazini Mashariki mwa nchini hiyo akiwa anakabiliwa na mashtaka 13, Ntaganda mwenye miaka 45 atasomewa hukumu July,8 Mwaka huu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad